IAM THE MUSIC

mercychiva

Classic rock at heart, yet I do have another side called Alternative. My characteristics are rock and roll. Folk is when I have something to say; rap is when I have a lot to say. My happiness shines through pop. I laugh through country, I cry through the blues, I dance through hip hop, and I sing through opera. Ambient– my nature, techno– my craziness, R&B– my love life, classical– my relaxation, emo– my anger, and gospel– my religion (which is practiced through reggae, my spirituality). Jazz is my superficiality. And for anyone special in my life, tango since two can tango (and they can salsa). Indie is my unheard of nature (and trust me, I am very often unheard). Punk is my rebellious self, which sprung through my deep dark secrets in heavy metal. Acoustic is when I am best heard, soft rock is when I am best known…

View original post 53 more words

Advertisements

TRENDING NOW

BUNGOMA COUNTY

Serikali ya kaunti ya Bungoma imewataka wanakandarasi waliopewa kazi katika kaunti hiyo kufutilia mbali mpango wao wa kuandaa maandamano kwa mwezi moja ikisema inashughulikia matakwa yao.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa barabara na ujenzi katika serikali ya kaunti hiyo, Stephen Nendela anayesema kuwa kutolipwa kwa wanakandarasi hao kumesababishwa na kucheleweshwa kutolewa kwa pesa hizo na serikali kuu.

Akizungumza alipokutana na wanakandarasi hao mjini Bungoma, Nendela amesema kuwa watawalipa wanakandarasi wote punde pesa hizo zitatolewa na serikali kuu

KAUNI YA VIHIGA

Serikali ya kaunti ya Vihiga imetenga shilingi millioni sabini kwa ujenzi wa taasisi ya mafunzo ya anuwai katika eneo bunge la Sabatia.

Akiongea wakati wa kuzindua mradi wa ujenzi wa taasisi hiyo, mbunge wa eneo hilo Alfred Agoi amesema kuwa ni afueni kwa wanafunzi wa eneo hilo ambao husafiri mwendo mrefu kutafuta elimu ya juu huku akiongeza kuwa taasisi hiyo pia itawapa nafasi wanafunzi ambao hawatapata nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu.

Wakati uo huo mkurungenzi wa bodi inayosimamia taasisi za kiufundi na vyuo vya kadri eneo la Magharibi, Joseph Sunguti amewaomba wazazi kuwapeleka watoto wao katika taasisi hiyo baada ya ujenzi wake kukamilika.

BUSIA COUNTY

Huku zoezi la kusajili wapiga kura kote nchini likitazamiwa kuanza mapema juma lijalo, wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Busia kujitokeza kwa wingi na kutafuta stakabathi hiyo muhimu ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.

Ni kauli iliyotolewa na baadhi ya waakilishi wa wadi katika kaunti ya Busia wakiongozwa na naibu spika wa bunge la kaunti hiyo Moses Ote ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Angurai Kusini na kiongozi wa walio wachache katika
bunge hilo Moses Mamai, wakisema kuwa hatua hiyo imelenga kuhakikisha kuwa inawapa idadi ya kutosha mbali na kuwa na usemi katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha wamewataka walimu wakuu kuhamasisha wanafunzi ambao wamehitimu kupokea vitambulisho kufanya hivyo ili kushiriki kwenye zoezi hilo.

Hata hivyo Mamai ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Ang’urai ya Kati, Teso Kaskazini amewataka wakaazi wa wadi hiyo ambao vitambulisho vyao vya kitaifa viko katika afisi za usajili kuvichukua ili waweze kupata fursa ya kujisajili kama wapiga kura.

 

Trending now

BUNGOMA COUNTY

Mwenyekiti wa walimu wakuu wilayani Bungoma Kaskazini, Rose Soita amewataka viongozi wa kisiasa kukoma kuweka mipaka katika maswala ya maendeleo shuleni

BUNGOMA COUNTY

Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakizidi kujiunga na shule za upili, baadhi yao waliopata alama ya juu hawajafanikiwa kujiunga na shule za kitaifa kama inavyotarajiwa kutokana na ukosefu wa karo.  

Haya ni kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya Matulo, Joyce Mulunda ambaye amesema kuwa wanafunzi wengi waliostahili kujiunga na shule za kitaifa wamejiunga na shule hiyo kwa kuwa kiwango cha karo ni cha chini ikilinganishwa na shule zingine.

Hata hivyo baadhi ya wazazi na wanafunzi tuliozungumza nao wamesema kuwa shule za mashinani zinawapa fursa nafasi nzuri ya kulipa karo pamoja na kuwa na uhusiano mzuri kati ya walimu na wazazi wakisema wakati mwingi wazazi wanawatembelea watoto wao na kufuatilia vile wanasoma

KAUNTI YA KAKAMEGA…

Vijana na akina mama wa chama cha TNA kaunti ya Kakamega wamezindua mikakati ya kushirikiana na tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuhakikisha kuwa wakaazi wa eneo hilo wanajitokeza kwa wingi na kujiandikisha kama wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu ujao

Kwenye mkutano uliowaleta pamoja mamia ya vijana na akina mama waliojitokeza kupokezwa elimu kuhusu umuhimu wa zoezi hilo ambalo litangoa nanga rasmi wiki lijalo, mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kakamega
Desmond Shinaka amesikitikia idadi ndogo ya watu waliojitokeza kujiandikisha kama wapiga kura

Naye katibu wa chama hicho Donald Musi amesema kuwa wameweka mikakati ya kutosha kuhakikisha kuwa rais Uhuru Kenyatta anasalia uongozini akihoji kuwa kando ya kuwa kijana ameyajali maslahi ya wakenya wote.

Naye kiongozi wa akina mama amabye pia alihudhuria hafla hiyo Bi.Abigael Makotsi amesifia huduma zinazotolewa na
serikali ya Jubilee na kuwataka akina mama kumuunga mkono rais kwa uchaguzi

 

KAUNTI YA KAKAMEGA…

Mshukiwa mmoja wa wizi wa piki piki ameuawa kwa kuchomwa katika mtaa wa Shikhambi mjini Kakamega baada ya jaribio lake la kuiba piki piki kugonga nanga hapo jana

Kulingana na walioshuhudia tukio hilo,mshukiwa huyo alikuwa miongoni mwa genge la watu tano waliojifanya abiria kabla ya kumvamia Pius Ondako aliyekuwa akitoka eneo la Mungulu majira ya saa kumi za asubuhi hapo jana kabla ya mhudumu huyo kupiga kamsa iliyovutia wananchi

Msako dhidi ya washukiwa wengine waliotoroka umeanza huku wakaazi wa eneo hilo wakilalamikia hali mbaya ya usalama baada ya kubainika kuwa zaidi ya watu nane wameuawa kwa njia tata katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wakiitaka serikali ya kaunti hiyo kuingilia kati kusaidia kuthibiti hali hiyo

 

KAKAMEGA COUNTY

 

Ukosefu wa wataalam wa kuunda miswada umetajwa kama sababu kuu ya uchache wa miswada iliyopitishwa kuwa sheria na bunge la kaunti ya Kakamega.

 

Akizungumza na wanahabari mjini Kakamega, spika wa bunge la kaunti ya Kakamega, Maurice Buluma ameeleza kuwa bunge hilo limepitisha jumla ya miswada 25 kuwa sheria tangu kuanzishwa kwake na kuhoji kuwa wengi wa wabunge hawana uzoefu wa kubuni miswada.

Kauli hii imeungwa mkono na mwakilishi wa wadi ya Kongoni aliyepia kiongozi wa wengi kwenye bunge hilo Robert Makhanu.

Naye kiongozi wa wachache kwenye bunge hilo Titus Kwoma amehoji kuwa ukosefu wa fedha na malumbano baina ya wabunge ndiyo imechangia bunge hilo kutopitisha baadhi ya miswada katika bunge hilo.

BUSIA COUNTY

Maafisa wa polisi mjini Busia wamenasa tani tatu za miti aina ya Saddle Wood yenye thamani ya shilingi milioni sita nukta nane iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea taifa la Uganda katika eneo la Tanaka.

Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi Kaunti ya Busia Bi. Halima Abdi amesema kuwa watu wawili waliokuwa wanasafirisha miti hiyo wametiwa mbaroni wakisubiri kufikishwa mahakanani.

Aidha Bi. Halima amelalamikia ongezeko la visa vya ulanguzi wa bidhaa hizo akiitaka idara ya mahakama kuhakikisha kesi hiyo inasikizwa na kuamuliwa kwa wakati ufaao ili kuwezesha idara hiyo kuharibu miti hiyo kwa mujibu wa sheria za kutunza mazingira nchni.

VIHIGA COUNTY

Mamia ya wakazi wa wadi ya Wemilabi eneo bunge la Luanda wamejitokeza kutuma maombi ya kupata vitambulisho vya kitaifa, shughuli inayofadhiliwa na mwanaharakati wa kisiasa kutoka eneo hilo Urthur Apungu.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa shughuli hiyo katika makao ya chifu wa eneo la Ebbayi, mwanaharakati huyo amesema kuwa amechukua jukumu hilo kuona kuwa kila mmoja anapata haki zake zikiwemo za kisiasa.

Apingu amedokeza kuwa ameweka mpango kuona kuwa kila mkazi ananufaika huku akiwataka wasipotoshwe na viongozi wasiotaka maendeleo eneo hilo na kuwataka washikiane na maafisa hao wa isajili.
Naye afisa wa usajili watu wilayani Emuhaya Charles Rading ametoa wito kwa watawala wa eneo hilo kuhamasisha wakazi umuhimu wa stakabadhi hiyo muhimu

BUNGE LAFUNGULIWA…

Mbunge wa Shinyalu, Anami Lisamula ametoa wito kwa wabunge kushirikiana na taasisi zilizotwikwa jukumu la kukabiliana na ufisadi nchini ili kusaidia kupunguza ongezeko la visa vya ufisadi nchini.

Akizungumza kwenye kikao cha bunge kilichoandaliwa hapo, Lisamula amesema kuwa ufisadi umeathiri ukuaji wa uchumi wa taifa hili na kuwa ni jukumu la wabunge kushirikiana na tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC katika vita hivyo.

Lisamula amesema kuwa bunge vile vile linastahili kushirikiana na afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kutambua na kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wakuu serikalini watakaopatikana wakijihusisha na ufisadi.

BUNGE LAREJELEA VIKAO VYAKE…

Bunge la kitaifa limefanyia marekebisho kamati ya shughuli za bunge huku wanachama watatu wakiondolewa.

Baadhi ya wanachama wapya walioidhinishwa ni pamoja na mbunge wa Matungu, David Were na mwenzake wa Kajiando Kusini, Katoo Ole Metito huku Khatib Mwashetani akiwa miongoni mwa wale waliotemwa kutoka kwenye kamati hiyo.

Spika wa bunge hilo Justin Muturi amewataka wanachama hao kuzingatia kanuni za kamati hiyo na kuwaonya dhidi ya kukosa kuhudhuria vikao vya kamati hiyo

Kamati zingine zitaendelea kusalia jinsi zilivyo baada ya idadi kubwa ya wabunge kupinga pendekezo la kufanyia kamati hizo mabadiliko ili kuimarisha utendakazi wake.

RUTO AKUTANA NA MAGAVANA…

Rais Uhuru Kenyatta hii leo ameratibiwa kuandaa mkutano na baraza la magavana nchini kujadili mikakati itakayohakikisha kuwa kuna usimamizi mzuri katika serikali kuu na zile za kaunti

Mkutano huo wa siku mbili utaandaliwa katika ikulu ndogo ya Sagana kaunti ya Kirinyaga na unajiri siku moja baada ya naibu rais William Ruto kukutana na baadhi ya magava katika makao yake ya Karen jijini Nairobi na kuzitaka serikali za kaunti kuhakikisha kuwa raslimali zinazotolewa na serikali ya kitaifa zinatumika kwa njia inayofaa.

mwisho……………………………..

TRENDING NOW

Mwenyekiti wa muungano wa walimu nchini KNUT Mudzo Nzili amesema kuwa kamwe hawatalegeza msimamo wao wa kutetea walimu humu  nchini licha ya serikali kujaribu kuwapiga vita.

Akizungmza katika eneo la Nyambene kaunti ya Meru ,Nzili amesema kuwa  tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC imefeli kutekeleza  ahadi wailoafikiana hapo awali ya nyongeza ya mishahara ya asilimia hamsini hadi sitini .

Kwa upande mwingine katibu mkuu wa muungano huo Wilson Sossion  ameipa serikali makataa ya hadi tarehe ishirini na saba mwezi huu kuandaa mazungumzu ya nyongeza ya mishahara na vyama vya walimu  la sivyo waandae mgomo wa kitaifa.

 

Spika wa bunge la seneti Ekwe Ethuro anaitaka serikali kuu kuboresha huduma za afya katika kaunti zote humu nchini ili kuwawezesha wananchi kuptata huduma bora za matibabu.

Ethuro amewataka wahudumu wa afya kushirikiana na serikali za kaunti ili kusuluhisha changamoto zinazo wakabili badala ya kuandaa migomo ya  mara kwa mara .

Hata hivyo amekashifu baadhi ya wauuguzi ambao huwapuuza wagonjwa wadharura kwa akisema hatua hiyo imesababisha vifo vya wakenya wengi.

 

 

TRENDING NOW IN WESTERN KENYA

KAUNTI YA KAKAMEGA

Mwakilishi wawanawake katika kaunti ya kakamega Rachel Ameso amesema kuwa wanafunzi mia moja na themanini  waliofanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwa jana watanufaika na ufadhili wa masomo ya kujiunga na kidato cha kwanza kutoka afisi yake.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari afisini mwake Ameseo  amesema kuwa afisi yake imetenga fedha za kutosha zitakazo fanikisha masomo ya watoto hao na kuongeza kuwa wanafunzi watatu  katika kila wadi kaunti hiyo waschana wawili na mvulana mmoja  watapata udhamini huo.

Aidha, Ameso  ametoa wito kwa viongozi wengine waliochaguliwa kuwasaidia watoto werevu wanaotoka jamii maskini

 KAUNTI YA KAKAMEGA

Mbunge wa Likuyani  Enock Kibunguchy ameitaka serikali ya kaunti ya Kakamega kukamilisha mradi wa usambazaji maji ambao umekwama kwa miaka miwili sasa.

Akizungumza lipozuru miradi ya CDF katika wadi ya Sinoko, Kibunguchy amemshtumu gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya kwa kuzindua mradi huo na kisha kushindwa kuukamilish na kuongeza kuwa hiyo ni ishara ya uongozi usio na mpangilio

Kibunguchy ameongeza kuwa kuna uwezekano kuwa shilingi milioni thelathini zilizotengewa mradi huo zimefujwa na kutaka walewate wanaohusika na mradi huo kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

KAUNTI YA KAKAMEGA

Chifu wa Kata ya Kongoni Wilayani Lugari Paul Makete ametoa wito kwa wakaazi wanaoishi mpakanai mwa kaunti ya kakamega na Uasin Gishu kudumisha amani ili kufanikisha maendeleo katika kaunti hizo mbili.

Akizungumza katika eneo hilo katika baraza la uma lililowaleta pamoja wazee kutoka jamii mbili za eneo hilo, wakaazi hao wamevilaumu vitengo vya usalama kwa kuzembea na kuruhusu wahalifu kupenya katika maeneo hayo huku wahudumu wa bodada wakiathirika zaidi kwa kuuawa na kuibiwa pikipiki zao.

Matamshi yake yanajiri wiki moja baada ya muhudumu mmoja wa piki piki eneo hilo kuuawa na wahalifu waliojifanya kuwa abiria huku wakaazi wa eneo hilo wakitishia kuchukulia sheria mikononi mwao ikiwa visa vya uhalifu havitadhibitiwa na maafisa wa polisi

TRENDING NOW

 

BUNGOMA COUNTY

Mwanamke mmoja kutoka kijiji cha S.A viungani mwa mji wa Webuye amepokea kichapo kutoka kwa wakaazi wa eneo hilo waliokuwa na ghadhabu baada ya kudaiwa kuwa amekuwa akimdhulumu mwanawe anayeishi na ulemavu na kumzuilia kwa zaidi ya miaka kumi na mitatu.

Wakaazi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa watu wanaoishi na ulemavu katika wilaya ya Bungoma Mashariki, Rebecca Khaemba wamemtia nguvuni mshukiwa kwa jina Elizabeth Akiru na kuwakabidhi maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Webuye.

 

Rebecca amewalaumu viongozi wa eneo hilo kwa kukosa kuchukulia hatua za kisheria watu wanaowatelekeza watoto wenye ulemavu na kuitaka serikali ya kuingilia kati na kuwasaidia.

Chifu wa kata ya Webuye Mjini, Barasa Misiko amedhibitisha kisa hicho na kuwatahadharisha wazazi walio na mazoea ya kuwatelekeza watoto wenye ulemavu kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

BUNGOMA COUNTY

Mwakilishi wadi ya Kimaeti katika bunge kaunti ya Bungoma, Simiyu Wechuli na mwenzake wa Kabuchai/Chwele, Barasa Mukhongo wameilaumu serikali ya kaunti hiyo kwa kuchelewa kutoa shilingi milioni ishirini na nane kwa wadi jinsi ilivyoahidi wakisema Gavana wa kaunti hiyo Kenneth Lusaka huzindua miradi kabla ya kupata pesa za kuifadhili.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Bungoma, wawili hao wamesema kuwa wakaazi wa kaunti ya Bungoma huenda wakawalaumu wawakilishi wadi kuwa wamepokea pesa hizo na kuzitumia vibaya huku wakiitaka serikali ya kaunti hiyo kuelezea sababu za kutotolewa kwa pesa hizo.

Hata hivyo wamesema kuwa wawakilishi wa wadi hawana uwezo wa kufuja pesa hizo na kuongeza kuwa sheria za matumizi ya pesa za maendeleo ziliidhinishwa na bunge la kaunti ya Bungoma ili kutoa mwelekeo jinsi ya kutumia pesa hizo na kuzuia matumizi mabaya.

 

BUNGOMA COUNTY

Mbunge wa Kimilili, Suleiman Murunga amewataka walimu wakuu wa shule za msingi na upili kutumia vyema fedha wanazopewa kutoka hazina ya CDF.

UASIN GISHU COUNTY

Mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu kaunti ya Uasin Gishu, David Ondolo amewalaumu wanajeshi wa kambi ya kijeshi ya Moi mjini Eldoret kwa kuwanyanyasa wakaazi wa eneo la Soi kwa kisingizio kuwa wanajeshi hao wanaomboleza vifo vya wenzao nchini Somalia.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari eneo hilo, Ondolo amesema kuwa wanajeshi hao wamekuwa wakiwapiga kiholela na kuwahangaisha wakaazi wa Soi jambo ambalo amesema limepelekea wakaazi hao kuishi kwa hofu.

Ondolo ameitaka wizara ya ulinzi kuingilia kati na kuchunguza swala hilo na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika baada ya mwanamme wa umri wa makamo kudaiwa kupigwa na wanajeshi wa kambi hiyo.

 WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA

Wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nane mwaka jana wanaanza kujiunga na shule za upili hii leo huku wanafunzi elfu mia saba hamsini na tisa mia sita na tatu wakitarajiwa kujiunga na shule mbalimbali za upili nchini.

Katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang’ amesema kuwa wanafunzi ambao hawatajiunga na shule walizoitwa, nafasi zao zitapeanwa kwa wanafunzi wengine baada ya muda uliowekwa kujiunga na shule za upili kukamilika terehe kumi mwezi huu.

Kipsang’ amesema kuwa wanafunzi laki saba hamsini na tisa, mia sita na tatu wanatarajiwa kujiunga na shule za upili mwaka huu

TUNOI KUJUA HATMA YAKE LEO

Kamati iliyoteuliwa kuchunguza madai ya ufisadi dhidi ya jaji wa mahakama ya upeo, Philip Tunoi inatarajiwa kuwasilisha ripoti yao hii leo kwa tume ya Huduma za mahakama, JSC.

Hii ni baada ya kuwahoji watu wanaodaiwa kuhusika na madai yake Tunoi kupokea hongo ya shilingi milioni mia mbili kutoka kwa gavana wa Nairobi Evans Kidero ili kumpendelea kwa kesi ya uchaguzi mkuu wa 2013.

Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wa tume ya utumishi wa umma, Margaret Kobia imewahoji jaji Tunoi, Kidero na wahusika wengine wanaodaiwa kuhusika na sakata hiyo.

Alipofika mbele ya kamati hiyo hapo jana, Kidero alikana madai hayo na kusema kuwa hajawahi kutana na jaji Tunoi ana kwa ana na kutishia kuwashtaki wanaomhusisha na sakata hiyo akiwemo wakili Amednasir Abdulahi ambaye amesema yuko tayari kupambana na Kidero mahakamani iwapo Kidero atamshitaki.

KIMATAIFA

Wanachama wa Republican na Democrats, Marekani wanaopigania tiketi za vyama vyao tayari kwa uchaguzi wa urais Marekani wameanza kuwasili katika jimbo la New Hampshire ambapo uchaguzi mwengine utafanyika.

Walioshinda katika kamati za wabunge za Iowa walikuwa Sineta Ted Cruz wa chama cha Republican na Hillary Clinton wa Democrats.

Cruz alishinda licha ya kuwa nyuma katika kura ya maoni huku Bi.Clinton akimshinda seneta Bernie Sanders kwa asilimia 0.2.

Jimbo la New Hampshire linaonekana kuwa na changamoto tofauti kwa vyama hivyo.

Jimbo hilo lenye watu wa msimamo wa kadri na wasio na wasiofuata dini huenda likawa changamoto kubwa kwa Cruz wakati mchujo huo utakapofanyika mnamo tarehe 9 mwezi Februari.

Donald Trump, ambaye amekuwa kifua mbele kwa upande wa chama cha Republican anatarajiwa kufanya vyema zaidi ya Iowa ambayo mchujo wa kwanza ulifanyika.

Upande wa Democrats, Sanders anaonekana kuwa na fursa ya kuwa nyumbani dhidi ya Bi Clinton, akiwa seneta wa jimbo jirani la Vermont.

Khalwale says he speaks out for the poor

Kakamega senator Bonny Khalwale during apst funeral in Mumias.PHOTOS JOIHN NALIANYA

KAKAMEGA Senator Bonny Khalwale has denied claims he is fond of insulting other Luhya leaders.

Speaking to the Star yesterday on the phone, he said Water CS Eugene Wamalwa said he is childish and abusive.

On Sunday in Bumula constituency, Wamalwa said abusive and confrontational politics is childish and in bad taste for a leader of Khalwale’s calibre.

“My defense for the rights of the poor Luhya people should not be misconstrued to mean I undermine other leaders,” Khalwale said

He said most Luhya governors misuse public funds.

“It is not strange that when I rebuke the rich for stealing from the poor they gang up to call me abusive,” Khalwale said.

The senator said what he told Vihiga Governor Moses Akaranga during the Akaranga’s sisters funeral on Saturday was the truth.

Khalwale said a report by the Auditor General had revealed Vihiga county had Sh2.5 billion debt, yet there were no visible projects.

On Saturday, the senator said he taught Akaranga about politics, as the governor was afraid of ANC leader Musalia Mudavadi.